Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama

( KUWASA )

Karibu

Allen Marwa photo
Bw. Allen Marwa
Mkurugenzi Mtendaji

: allen.marwa2@kuwasa.go.tz

: +255767309140

KUWASA ilianzishwa tarehe 21 Juni 2002 kwa mujibu wa Sheria ya Waterworks, Sura ya 272, ikiwa na jukumu la kuendesha na kusimamia huduma za majisafi na usafi wa mazingira. Kwa sasa, Mamlaka inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2009, pamoja na sheria, kanuni, sera na viwango vinavyosimamia sekta ya maji nchini.

Mamlaka inafanya kazi chini ya usimamizi wa Wizara ya Maji na inadhibitiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

KUWASA ipo katika daraja "A". Hii ikimaanisha kuwa ina wajibu wa kugharamia shughuli zote za kiutendaji na Maboresho ya huduma.Hata hivyo Chanzo chetu kikubwa cha maji ni Ziwa Victoria ambako maji yanasafirishwa kwa umbali wa kilomita 117 kutoka kwenye chanzo mpaka Kahama kwa njia ya mseleleko wa asili (gravitation force) kupitia mabomba yenye vipenyo vya milimita 1200, 1100, na 750 na baada ya hapo upokelewa kwenye tangi kuu lakuhifadhia Maji kwa lengo la kuyasambaza kwa wateja ili yaweze kutumika. 

 Uzalishaji wa maji wa KUWASA unategemea kwa kiasi kikubwa ununuzi wa maji ya jumla (bulk water) kutoka kwa Mamlaka ya Majisafi Kahama Shinyanga (KASHWASA), ambayo inavuta maji kutoka Ziwa Victoria kupitia mtambo wa Ihelele. Maji hayo yaliyosafishwa tayari husafirishwa kupitia bomba kuu la kitaifa na kupokelewa kwenye matanki makubwa ya uhifadhi ya KUWASA yaliyopo mjini Kahama kabla ya kusambazwa kwenye mitandao ya miundombinu ya maji ya reja reja kwa ajili ya majumbani, taasisi, na viwanda.

 Kutokana na ukuaji wa kasi wa eneo la Manispaa ya Kahama kama kitovu cha biashara na uchimbaji wa madini, KUWASA inatekeleza miradi ya upanuzi wa mtandao wa mabomba ili kufikia maeneo mapya yaliyotengwa kwa ajili ya makazi na viwanda vidogo vidogo. Mamlaka pia inatunza baadhi ya visima virefu vya asili kama vyanzo vya dharura ili kuhakikisha usalama wa upatikanaji wa maji unakuwa wa uhakika wakati wote hata pale ambapo kuna matengenezo kwenye bomba kuu la kitaifa kutoka Ziwa Victoria.

slot gacor