Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA)
- Sample Data-Articles
Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Kahama ilianzishwa mnamo tarehe 21 Juni 2002 kwa sheria ya "water works Act cap 272" iliyofanyiwa marekebisho na sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2009.
KUWASA ipo katika daraja A. Hii ikimaanisha kuwa ina wajibu wa kugharamia shughuli zote za kiutendaji na Maboresho ya Huduma Chanzo chetu cha maji ni Ziwa Victoria ambako maji yanasafirishwa kwa umbali wa kilomita 117 kutoka kwenye chanzo kwa kutumia mabomba yenye vipenyo vya milimita 1200, 1100, na 750.
Dira Yetu
Kuwa Mamlaka Bora katika kutoa huduma endelevu za Majisafi na Usafi wa Mazingira Nchini Tanzania.
Dhima Yetu
Kutoa huduma bora na endelevu za majisafi na usafi wa mazingira zinazokidhi vigezo kimataifa kwa bei nafuu.