Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama

( KUWASA )

Kuhusu sisi

Mamlaka Ya MajiSafi Na Usafi Wa Mazingira Kahama (KUWASA)

KUWASA ilianzishwa mnamo tarehe 21 Juni 2002 kwa sheria ya "water works Act cap 272" iliyofanyiwa marekebisho na sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2009.

KUWASA ipo katika daraja A. Hii inamaanisha kuwa Mamlaka ina wajibu wa kugharamia shughuli zote za kiutendaji na Maboresho ya Huduma.

Chanzo chetu cha Maji

Chanzo chetu cha maji ni Ziwa Victoria ambako maji yanasafirishwa kwa umbali wa kilomita 117 kwa mabomba.

Dhima Yetu

Kuhakikisha huduma za maji na usafi wa mazingira zinatolewa kwa usalama, kwa njia endelevu, kwa ufanisi, na kwa usawa kwa bei nafuu ili kuhakikisha uendelevu wa mradi.

Dira Yetu

Kuwa Mamlaka Bora katika kutoa huduma  ya Majisafi na Usafi wa Mazingira  Tanzania.

Misingi Ya Utendaji Wetu

1. Kutimiza Dira na Dhima ya Mamlaka.
2. Kuboresha na Kukuza Ushirikiano na Kujituma
3. Uwazi
4. Ukweli
5. Uwajibikaji.
6. Wateja Kwanza
7. Watumishi ni Rasilimali namba moja ya Mamlaka
8. Kuwajibika kwa jamii inayotuzunguka
9. Wafanyakazi kuhimizwa kujifunza na kubadilishana maarifa

Malengo Yetu

  1. Kuboresha Upatikanaji wa MajiSafi na Salama
  2. Kuboresha makusanyo ya mwezi ya huduma ya Majisafi
  3. Kuboresha utunzwaji wa Mazingira na Uhifadhi wa vyanzo vya maji
  4. Kuboresha makusanyo ya mwezi ya huduma ya Majitaka
  5.  Kufanikisha kuboresha na kuongezwa kwa sheria ya MajiSafi na Usafi wa mazingira.