Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama

( KUWASA )

Njia za malipo

 

 

Namna ya Kulipa Ankara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama(KAHAMA UWASA) inapenda kuwafahamisha watumiaji wa huduma za maji kua kwa sasa malipo yote ya ankara za maji yafanyike kwa njia zifuatazo:-

🏦  Kupitia Mawakala wa Benki

Mteja atatakiwa kufika kwa wakala wa Benki aliye karibu naye na kumpatia Nambari ya Malipo (Control Number) iliyo kwenye mfumo huu "994770xxxxxx" ambayo ina tarakimu 12 na kiwango cha pesa ambacho anataka kulipia huduma ya maji. Wakala atathibitisha taarifa zake kwenye mfumo na kumpatia risiti kwa malipo aliyofanya.

📱 Kupitia huduma ya simu (MPESA, T-Pesa, Airtel Money, HALOPESA, Tigo Pesa)

Kupitia njia ya simu ya mkononi kwa mitandao ya simu. Mteja aingie kwenye Malipo ya Serikali kisha aingize namba ya malipo (Control Number) na kuweka kiasi na kuthibitisha, Mfano kulipa kwa Mpesa:-.

Mteja anaweza kulipia ankara ya maji kwa mawakala wote wa Benki za Posta, NMB, NBC, na CRDB na Kupitia mitandao ya simu kwa huduma za MPESA, AIRTEL MONEY, TTCL PESA, EASY PESA, na HALOPESA. Ili kuweza kufanya malipo, ni lazima kuwa na Namba ya Malipo (Control Number) ina tarakimu kumi na mbili (Mfano: 994770611287). Kulipa kwa simu fuata hatua hizi:-

  1. Bonyeza: *150*00# ili kuingia kwenye menyu ya MPESA (Mitandao mingine fuata code namba husika)
  2. Bonyeza namba 4 (Lipa kwa Mpesa)
  3. Bonyeza namba 5 (Malipo ya Serikali)
  4. Bonyeza namba 1 (Weka namba ya kumbukumbu)

Ingiza namba yako ya Malipo yaani Control Number (Mfano:  994770611287 )

  1. Ingiza Kiasi
  2. Ingiza namba yako ya Siri ili kuthibitisha malipo kwenda KAHAMA  URBAN WATER SUPPLY AND SANITATION AUTHORITY
  3. Bonyeza  1 kufanya malipo
  4. Au Bonyeza 2 kubatilisha.

✅ N.B/  Baada ya kufanya malipo utapokea ujumbe kutoka kwetu KAHAMAUWASA utakaothibitisha malipo yako kutufikia.

📩  Kufahamu Ankara Yako

Kila mwanzoni mwa mwezi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama hutoa Ankara (Bili) za maji kwa wateja na kuzituma kwa njia ya meseji fupi (SMS). Ikiwa mteja hajatumiwa Ankara kwa mwezi husika, anaombwa kupiga simu ofisini na aweze kupewa Ankara yake ya Maji  na hivyo kulipia Ankara husika kwa wakati.

⚠️ Kusitishiwa Huduma

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama itasitisha huduma ya maji kwa mteja endapo hatafanya yafuatayo

  • Kushindwa kulipa ankara (bili) ya kila mwezi
  • Kuiba maji kwa namna yoyote mfano:- kujiungajishia maji kinyume na utaratibu, kuharibu dira ili isisome vizuri, kukata bomba linalota maji n.k
  • Ikabainika kua mteja amesababisha mivujo ya maji kwa makusudi.

Hivyo Mamlaka inawasisitiza wateja kufuata taratibu zilizowekwa za kuunganisha maji na kulipia ankara za maji kila mwezi ili kuepuka gharama na adhabu zinazosababishwa na kusitishiwa huduma.

Kwa msaada zaidi tafadhali piga simu ya ofisini bure kwa namba: 0800110320 au 0800110321

slot gacor