The United Republic of Tanzania
Ministry of Water

Kahama Water Supply and Sanitation Authority

( KUWASA )

Procedure for New Water Connection

 

 

UTARATIBU WA MAUNGANISHO MAPYA

 1. Fomu ya maombi

  • Mteja anapaswa kujaza fomu ya maombi ambayo inapatikana bure ofisi kuu ya KUWASA, kwenye tovuti ya KUWASA na kutoka ofisi zote za kanda.
  • Fomu iwe na mhuri kutoka ofisi ya Mtendaji au Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa.

2. Viambatisho vinavyohitajika  

  • Barua ya Afisa Mtendaji au Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa eneo husika
  • Picha mbili (Passport Size)
  • Nakala ya kitambulisho (Kitambulisho cha Taifa, Kadi ya Mpiga kura, Leseni ya udereva ama kitambulisho kingine kinachotambulika na serikali)
  • Kwa taasisi/mashirika watapaswa kupiga muhuri sehemu ya picha na kuweka viambatisho vya usajili wa taasisi/mashirika yao.

3. Upimaji (Survey) 

  • KUWASA itafanya upimaji kwa mteja aliyekamilisha kujaza fomu ya maombi na viambatisho vinavyohitajika na kuiwasilisha ofisi za KUWASA ndani ya siku saba za kazi.

4. Makadirio ya Gharama  

  • KUWASA itaandaa gharama zote za makadirio zinazohitajika kwa ajili ya maunganisho mapya.
  • Ununuzi wa vifaa vipya vya kuunganisha huduma ya maji itafanywa na KUWASA kwa kufuata sheria na kanuni za manunuzi ya umma.

5. Taarifa kwa mteja. 

  • Baada ya makadirio ya gharama, KUWASA itamjulisha mwombaji kupitia ujumbe mfupi (SMS) jumla ya gharama ya maunganisho. Gharama hizi pia zitapatikana kwa mteja kufika ofisi za KUWASA.

6. Malipo 

  • Makadirio ya gharama yatalipwa na mteja kupitia namba ya malipo ya serikali – Control Number, au utaratibu utakaowekwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

7. Utekelezaji wa maunganisho mapya.

  • Baada ya mteja kukamilisha malipo ya gharama za maunganisho mapya KUWASA itamfanyia mteja maunganisho ya huduma ya majisafi.
  • Baada ya maunganisho kukamilika KUWASA itafanya majaribio ya kuhakiki ufanisi wa maunganisho.
  • Dira ya maji itafungwa kwa mteja bure.