Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama

( KUWASA )

Huduma ya Majisafi

TARATIBU ZA MAOMBI YA MAUNGANISHO MPYA YA MAJI

Waombaji wanatakiwa kufuata taratibu hizi kikamilifu na si vinginevyo.

1. Maombi
Waombaji wanatakiwa kujaza fomu ya maombi inayopatikana mtandaoni kupitia:
https://huduma.maji.gov.go.tz/ au kuipata kupitia namba ya huduma kwa wateja ya KUWASA: "0800110320 / 0800110321" au tovuti ya KUWASA.

2. Nyaraka Zinazohitajika
• Barua ya utambulisho kutoka kwa Mtendaji wa Serikali ya Mtaa/Kijiji au Mwenyekiti au nyaraka ya umiliki wa eneo.
• Picha mbili (2) ndogo za pasipoti
• Nakala ya kitambulisho halali (NIDA, Kitambulisho cha Mpiga Kura)
Taasisi/mashirika lazima yaweke muhuri rasmi na kuambatanisha nakala za vyeti vya usajili.

3. Ukaguzi wa Eneo (Site Survey)
KUWASA itafanya ukaguzi wa eneo ndani ya siku tano (5) za kazi baada ya kuwasilishwa kwa fomu iliyojazwa kikamilifu pamoja na nyaraka zote zinazohitajika.

4. Makadirio ya Gharama
KUWASA itatayarisha makadirio ya gharama za uunganisho mpya.
Vifaa vyote vitanunuliwa na KUWASA kwa kuzingatia sheria na kanuni za ununuzi wa umma.

5. Taarifa kwa Mteja
Waombaji watajulishwa gharama kamili ya uunganishwaji kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS) au kupitia ofisi za KUWASA.

6. Malipo
Malipo yatafanywa kupitia Namba ya Malipo ya Serikali (Control Number).

7. Utekelezaji wa Uunganisho
Baada ya kuthibitisha malipo yote, KUWASA itatoa maelekezo kwa mteja na kuendelea na usakinishaji wa huduma ya maji.
Mita ya maji itatolewa na kufungwa bila malipo.

MUDA WA HUDUMA
• Baada ya kufanya malipo, mteja atapatiwa huduma ndani ya siku saba (7), au siku kumi na nne (14) kwa maeneo yanayohitaji upanuzi wa mtandao wa mabomba.
• Ikiwa kutakuwa na sababu zisizoepukika zitakazochelewesha utoaji wa huduma, Mamlaka itatoa taarifa rasmi.
• Ikiwa mteja hataridhika na huduma iliyotolewa, ana haki ya kuwasilisha malalamiko kwa Afisa Uhusiano.
• Mteja anahimizwa kutoa mrejesho baada ya kupokea huduma na kufuata maelekezo atakayopewa.

TAHADHARI
• Mamlaka haitahusika na makubaliano au malipo yoyote yatakayofanywa nje ya taratibu zilizowekwa na Mamlaka.

Ikiwa una maswali yoyote kuhusu maelezo haya, tafadhali fika ofisini au piga simu za ofisi kwa msaada zaidi.

 

slot gacor