Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama

( KUWASA )

Kuhusu Ankara

06 July, 2025

Namna ya Kulipa Ankara

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama, inapenda kuwafahamisha watumiaji wa huduma za maji kua kwa sasa malipo yote ya ankara za maji yafanyike kwa njia zifuatazo:-

    • Kupitia Mawakala wa Benki

Mteja atatakiwa kufika kwa wakala wa Benki aliye karibu naye na kumpatia Nambari ya Malipo (Control Number) iliyo kwenye mfumo huu "994770xxxxxx" ambayo ina tarakimu 12 na kiwango cha pesa ambacho anataka kulipia huduma ya maji. Wakala atathibitisha taarifa zake kwenye mfumo na kumpatia risiti kwa malipo aliyofanya.

    • Kupitia huduma ya simu (MPESA, T-Pesa, Airtel Money, HALOPESA, Tigo Pesa)

Kupitia njia ya simu ya mkononi kwa mitandao ya simu. Mteja aingie kwenye Malipo ya Serikali kisha aingize namba ya malipo (Control Number) na kuweka kiasi na kuthibitisha, mfano kulipa kwa Mpesa:-.

    1. Bonyeza: *150*00# ili kuingia kwenye menyu ya MPESA
    2. Bonyeza namba 4 (Lipa kwa Mpesa)
    3. Bonyeza namba 5 (Malipo ya Serikali)
    4. Bonyeza namba 1 (Ingiza Namba ya malipo)
    5. Weka tarakimu 12 zinazokuja na ankara yako
    6. Ingiza kiasi (mfano: 20500)
    7. Weka namba ya siri
    8. Thibitisha kwa kubonyeza 1

N.B Baada ya kufanya malipo utapokea ujumbe kutoka kwetu KAHAMAUWASA utakaothibitisha malipoyako kutufikia.

 

Kufahamu Ankara Yako

Kila mwanzoni mwa mwezi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama hutoa Ankara (Bili) za maji kwa wateja na kuzituma kwa njia ya meseji fupi (SMS). Ikiwa mteja hajatumiwa Ankara kwa mwezi husika, anaombwa kufika ofisini ili kuangalia taarifa zake na kulipia Ankara husika.

Kusitishiwa Huduma

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama itasitisha huduma ya maji kwa mteja endapo atafanya yafuatayo

  • Kushindwa kulipa ankara (bili) ya kila mwezi
  • Kuiba maji kwa namna yoyote mfano:- kujiungajishia maji kinyume na utaratibu, kuharibu dira ili isisome vizuri, kukata bomba linalota maji n.k
  • Ikabainika kua mteja amesababisha mivujo ya maji kwa makusudi

Hivyo Mamlaka inawasisitiza wateja kufuata taratibu zilizowekwa za kuunganisha maji na kulipia ankara za maji kila mwezi ili kuepuka gharama na adhabu zinazosababishwa na kusitishiwa huduma.