Barua Pepe: info@kuwasa.go.tz  Simu (BURE): 0737 804 270 | 0737 804 271

Namna ya Kulipa Ankara

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama, inapenda kuwafahamisha watumiaji wa huduma za maji kua kwa sasa malipo yote ya ankara za maji yafanyike kwa njia zifuatazo:-

    • Kupitia Mawakala wa Benki

Mteja atatakiwa kufika kwa wakala wa Benki aliye karibu naye na kumpatia Nambari ya Malipo (Control Number) iliyo kwenye mfumo huu "994770xxxxxx" ambayo ina tarakimu 12 na kiwango cha pesa ambacho anataka kulipia huduma ya maji. Wakala atathibitisha taarifa zake kwenye mfumo na kumpatia risiti kwa malipo aliyofanya.

    • Kupitia huduma ya simu (MPESA, T-Pesa, Airtel Money, HALOPESA, Tigo Pesa)

Kupitia njia ya simu ya mkononi kwa mitandao ya simu. Mteja aingie kwenye Malipo ya Serikali kisha aingize namba ya malipo (Control Number) na kuweka kiasi na kuthibitisha, mfano kulipa kwa Mpesa:-.

    1. Bonyeza: *150*00# ili kuingia kwenye menyu ya MPESA
    2. Bonyeza namba 4 (Lipa kwa Mpesa)
    3. Bonyeza namba 5 (Malipo ya Serikali)
    4. Bonyeza namba 1 (Ingiza Namba ya malipo)
    5. Weka tarakimu 12 zinazokuja na ankara yako
    6. Ingiza kiasi (mfano: 20500)
    7. Weka namba ya siri
    8. Thibitisha kwa kubonyeza 1
N.B Baada ya kufanya malipo utapokea ujumbe kutoka kwetu KAHAMAUWASA utakaothibitisha malipoyako kutufikia.

 

Kufahamu Ankara Yako

Kila mwanzoni mwa mwezi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama hutoa Ankara (Bili) za maji kwa wateja na kuzituma kwa njia ya meseji fupi (SMS). Ikiwa mteja hajatumiwa Ankara kwa mwezi husika, anaombwa kufika ofisini ili kuangalia taarifa zake na kulipia Ankara husika.

Kusitishiwa Huduma

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama itasitisha huduma ya maji kwa mteja endapo atafanya yafuatayo
  • Kushindwa kulipa ankara (bili) ya kila mwezi
  • Kuiba maji kwa namna yoyote mfano:- kujiungajishia maji kinyume na utaratibu, kuharibu dira ili isisome vizuri, kukata bomba linalota maji n.k
  • Ikabainika kua mteja amesababisha mivujo ya maji kwa makusudi
Hivyo Mamlaka inawasisitiza wateja kufuata taratibu zilizowekwa za kuunganisha maji na kulipia ankara za maji kila mwezi ili kuepuka gharama na adhabu zinazosababishwa na kusitishiwa huduma.

 

Usomaji wa Dira

Usomaji wa dira hufanyika kuanzia tarehe 15 hadi tarehe 23 ya kila mwezi. Zoezi hili hufanyika kwa watumishi wa Mamlaka kupita kwa wateja ili kuchukua taarifa mpya za dira. Uniti ambazo mteja wa huduma ya maji ambazo atakua ametumia hukokotelewa kwa kuchukua tofauti ya usomaji mpya kutoa usomaji wa zamani.
Wakati wa zoezi zoezi la kusoma dira watumishi wa Mamlaka huchukua taarifa zingine za dira kama dira kusoma tofauti au kama kuna uharibu wowote wa dira n.k.
Tunaomba wateja kuzingatia yafuatayo:-

  • Kutoa ushirikiano kwa wasomaji dira
  • Kwa wateja ambao dira zao zipo ndaji ya uzio, mtu awepo kwa kipindi hicho cha usomaji wa dira
  • Kuripoti tatizo lolote linalohusu dira kwa msomaji dira

Kusitishiwa Huduma

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama itasitisha huduma ya maji kwa mteja endapo atafanya yafuatayo

  • Kushindwa kulipa ankara (bili) ya kila mwezi
  • Kuiba maji kwa namna yoyote mfano:- kujiungajishia maji kinyume na utaratibu, kuharibu dira ili isisome vizuri, kukata bomba linalota maji n.k
  • Ikabainika kua mteja amesababisha mivujo ya maji kwa makusudi

Hivyo Mamlaka inawasisitiza wateja kufuata taratibu zilizowekwa za kuunganisha maji na kulipia ankara za maji kila mwezi ili kuepuka gharama na adhabu zinazosababishwa na kusitishiwa huduma.

Malengo yetu

1. Kuboresha Upatikanaji wa MajiSafi na Salama
2. Kuboresha makusanyo ya mwezi ya huduma ya Majisafi
3. Kuboresha utunzwaji wa Mazingira na Uhifadhi wa vyanzo vya maji
4. Kuboresha makusanyo ya mwezi ya huduma ya Majitaka
5. Kufanikisha kuboresha na kuongezwa kwa sheria ya MajiSafi na Usafi wa mazingira.

Misingi ya utendaji wetu

1. Kutimiza Dira na Dhima ya Mamlaka.
2. Kuboresha na Kukuza Ushirikiano na Kujituma
3. Uwazi
4. Ukweli
5. Uwajibikaji.
6. Wateja Kwanza
7. Watumishi ni Rasilimali namba moja ya Mamlaka
8. Kuwajibika kwa jamii inayotuzunguka
9. Wafanyakazi kuhimizwa kujifunza na kubadilishana maarifa

 

Dira Yetu

Kuwa Mamlaka Bora katika kutoa huduma endelevu za Majisafi na Usafi wa Mazingira Nchini Tanzania.

Dhima Yetu

Kutoa huduma bora na endelevu za majisafi na usafi wa mazingira zinazokidhi vigezo kimataifa kwa bei nafuu.

Chanzo cha Maji

Chanzo chetu cha maji ni Ziwa Victoria ambako maji yanasafirishwa kwa umbali wa kilomita 117 kwa mabomba

 
Go to Top