Maunganisho Mapya
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Kahama ina utaratibu maalumu wa kufuatwa kwa wateja ambao watahitaji huduma ya kuunganishiwa majisafi na majitaka. Utaratibu huo ni kama ifuatavyo.
Mteja anaehitaji huduma ya maunganisho ya maji atahitajika kufika ofisini za Mamlaka na kujaza fomu ya maombi.
Baada ya kujaza fomu watumishi wa Mamlaka watamtaarifu mteja siku ya kufanya ziara kwenye eneo lake na kupima vifaa na miundo mbinu itakayo tumika mpaka kufikishiwa huduma.
Mteja ataambiwa gharama za kuunganishiwa maji na vifaa ambazo atatakiwa kuzilipa katika ofisi za Mamlaka.
Mtejia ataunganishiwa Maji na kuanza kutumia huduma
ANGALIZO: Gharama zote za maunganisho ya maji zitalipwa katika ofisi za Mamlaka. Kwa msaada zaidi tunaomba ufike Ofisini kwetu Tafadhali