Ufuatao ni utaratibu wa kuomba huduma ya Majisafi katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Kahama.
Tunaomba waombaji wazingatie utaratibu huu na si vingenevyo.
Hatua za kufuata
1. Mteja atafanya maombi ya kuanganishiwa huduma ya maji kwa kujaza Fomu zinazopatikana Ofisi ya Mamlaka.2. Fomu itasainiwa na Afisa Mtendaji/Mwenyekiti wa eneo husika.
3. Baada ya hapo mteja ataiwasilisha fomu Ofisi ya Mamlaka.
4. Wataalam wa Mamlaka watafanya ukaguzi (Survey) kwenye eneo/nyumba inayoombewa huduma ya maji na kutayarisha gharama zinazohitajika katika maunganisho hayo.
5. Gharama zote zinazohusika zitalipwa Mamlaka ya Maji na mteja atapewa risiti inayolingana na malipo aliyofanya.
Taarifa muhimu za mteja
- Mteja anapaswa kutoa majina yake kamili (majina matatu)
- Anwani ya eneo analotoka/ au mtaa anaoishi
- Hati ya nyumba au kiwanja anachokiombea huduma ya maji
- Namba ya simu
- Kitambulisho cha Taifa/Leseni ya udereva/kitambulisho cha Kupiga kura au Kitambulisho cha kazi.
Muda wa Huduma
- Mteja akifanya malipo ya gharama za kuunganishiwa huduma atastahili kupatiwa huduma hiyo ndani ya siku saba kuanzia tarehe atakayokuwa amefanya malipo au siku kumi na nne eneo ambalo linahitaji kuendeleza bomba.
- Iwapo kutakuwa na sababu zisizozuilika zitakazofanya mteja asipate huduma katika muda uliopangwa, Mamlaka itampa mteja taarifa rasmi.
- Endapo mteja hatakua ameridhika na huduma atakayopewa ana haki ya kuwasilisha malalamiko yake kwa Afisa Uhusiano.
- Mteja atatoa taarifa mara baada ya kupata huduma na ushauri kwa huduma aliyopewa.
TAHADHARI
Mamlaka haitahusika na mapatano au malipo yoyote yatakayofanywa nje ya utaratibu uliowekwa na Mamlaka.Ukiwa na maulizo yoyote kuhusu maelezo haya Tafadhali fika Ofisini kwetu