Malengo Yetu
1. Kuboresha Upatikanaji wa MajiSafi na Salama
2. Kuboresha makusanyo ya mwezi ya huduma ya Majisafi
3. Kuboresha utunzwaji wa Mazingira na Uhifadhi wa vyanzo vya maji
4. Kuboresha makusanyo ya mwezi ya huduma ya Majitaka
5. Kufanikisha kuboresha na kuongezwa kwa sheria ya MajiSafi na Usafi wa mazingira.
Ankara
Kila mwanzoni mwa mwezi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama hutoa Ankara (Bili) za maji kwa wateja na kuzituma kwa njia ya meseji fupi (SMS). Ikiwa mteja hajatumiwa Ankara kwa mwezi husika, anaombwa kufika ofisini ili kuangalia taarifa zake na kulipia Ankara husika. Aidha wateja wanaweza kufahamu Ankara zao kwa kubonyeza ukurusa ufuatao.