Barua Pepe: info@kuwasa.go.tz  Simu (BURE): 0737 804 270 | 0737 804 271

Matumizi Bora ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA) imegundua malalamiko mengi ya wateja yanayohusu bili (Ankara) zao kua kubwa. Baada ya uchunguzi imegundulika kua ongezeko la bili za wateja linasababishwa na:
  • Bomba linalodondosha maji kwa matone mfululizo
  • Maji yanayovuja katika mtandao wa mabomba ya ndani
  • Maji yanayotiririka mfululizo kutokana na kuharibika kwa boya la choo cha kuvuta
  • Kufua kwenye bomba na maji yakiwa yanaendelea kutiririka
  • Kupiga mswaki huku bomba la maji likiwa linaendelea kutoa maji
  • Kutofundisha watoto matumizi bora ya maji
  • Kutumia majisafi na salama kwa ajili ya kumwagiia bustani, maji ya umwagiliaji si rahisi kuyakadiria (inashauriwa kutumia ndoo ya kumwagilia)
  • Kuosha vyombo wakati maji yanaendelea kutiririka.

Misingi ya utendaji wetu

1. Kutimiza Dira na Dhima ya Mamlaka.
2. Kuboresha na Kukuza Ushirikiano na Kujituma
3. Uwazi
4. Ukweli
5. Uwajibikaji.
6. Wateja Kwanza
7. Watumishi ni Rasilimali namba moja ya Mamlaka
8. Kuwajibika kwa jamii inayotuzunguka
9. Wafanyakazi kuhimizwa kujifunza na kubadilishana maarifa

 

Dira Yetu

Kuwa Mamlaka Bora katika kutoa huduma endelevu za Majisafi na Usafi wa Mazingira Nchini Tanzania.

Dhima Yetu

Kutoa huduma bora na endelevu za majisafi na usafi wa mazingira zinazokidhi vigezo kimataifa kwa bei nafuu.

Chanzo cha Maji

Chanzo chetu cha maji ni Ziwa Victoria ambako maji yanasafirishwa kwa umbali wa kilomita 117 kwa mabomba

 
Go to Top